Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesisitiza Uongozi wa Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea kutoa elimu ya ujasirimiamali kwa Vikundi ili kuwawezesha na kujua mtaji unawapa faida. RC Ibuge ametoa msisitizo huo wakati akizungumza kwenye kikao maalum cha CAG cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Madaba
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wote walihusika na ubadhirifu wa ujenzi, mradi wa hospitali ya Halmashauri ya Madaba na kwamba ametoa siku 60 mradi huo kukamilika kwa asilimia 100.Serikali imetoa shilingi bilioni 1.8 kutekeleza mradi huo.
Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma zimepata hati safi kufuatia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali katika mwaka unaoishia Juni 30 2021.Akizungumza katika kikao maalum cha CAG cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Madaba,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameipongeza Halmashauri hiyo kuungana na Halmashauri nyingine za Mkoa wa Ruvuma kuweza kupata hati safi kufuatia ukaguzi wa CAG na kwamba Halmashauri ya madaba pia imefanya vizuri katika utoaji mikopo kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.Show less
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa