MKUU wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile ametoa rai kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kulima zao la Ngano
Akizungumza na wananchi hao amesema ofisi ya Mkuu wa Wilaya imezungumza na kampuni ya bia ya Serengeti ambao watanunua zao hilo mara baada ya mavuno.
“Mwaka huu nimebuni na nyie mnatakiwa kuniunga mkono tutawapeni mbegu bure na tutafanya maarifa mpate na mbolea yeyote ambae anaheka moja na kuendelea tutampa mbegu na soko tunalo ni kampuni ya Bia ya Serengeti”.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuhimiza utunzaji wa misitu na kilimo cha ngano ikiwa wananchi wa Wino miaka 30 iliyopita walikuwa wanalima ngano kutokana na kutokuwa na soko waliacha kilimo hicho.
“Lakini kwa maelekezo mazuri ya Mkuu wa Wilaya kwamba ataleta mbegu na wanunuzi wa zao la ngano tunaomba swala hili lifanyike kwa haraka ili wananchi waweze kulima kwa wakati”.
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 16,2025.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa