Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba kwa kushirikiana na watendaji wa kata kuanza msako wa nyumba kwa nyumba kuwatafuta wanafunzi wa sekondari ambao hadi sasa hawajaripoti katika shule walizopangiwa Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la madiwani Halmashauri ya Madaba Mheshimiwa Mgema ameagiza hadi kufikia mwishoni mwa Januari mwaka huu wanafunzi wote wawe shuleni.Awali akitoa taarifa ya mahudhurio ya wanafunzi wa sekondari,Afisa Elimu Sekondari Maternus Ndumbaro amewataja jumla ya wanafunzi 1269 walipangwa katika shule za sekondari kuanza kidato cha kwanza ambapo hadi kufikia Januari 19,2023 ni wanafunzi 535 ndiyo wameripoti sawa na asilimia 42 ambapo asilimia 58 ya wanafunzi bado hawajaripoti.
“Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema hayupo tayari kuliingiza Taifa kwenye njaa kwa kuendekeza wafugaji na kwamba ni marufuku wafugaji kuingia kwenye maeneo ya wakulima.Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea Kanali Thomas amesisitiza kuwa Mkoa wa Ruvuma sio Mkoa wa wafugaji bali ni Mkoa wa kilimo ambao unaongoza kitaifa kwa kuzalisha mazao ya chakula .
KATA ya Lituta Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma inatekeleza mradi wa sekondari mpya ya mfano kupitia mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP)ambapo serikali kupitia mradi huo imetoa shilingi milioni 470.MKuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekagua mradi huu .Katika Mkoa wa Ruvuma zinajengwa shule za sekondari 11 kupitia mradi wa SEQUIP kwa gharama ya shilingi bilioni 7.7
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa