Halmashauri ya Wilaya ya Madaba itaanza rasmi zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpigakura Januari 28,2025 hadi Februari 3,2025.
Hayo amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ambaye ni Afisa mwandikishaji Jimbo la Madaba Sajidu Idrisa Mohamed.
Akizungumza katika kikao cha mapitio ya mpango mkakati wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele amesema zoezi hilo litafanyika kwa mujibu wa ratiba kwa wale ambao hawakufikisha umri wa miaka 18,waliohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuondoa wale ambao wametangulia mbele za haki pamoja na wale taarifa zao zilikosewa.
“Niwahamasishe na ninyi mkawe mabalozi katika maeneo yenu wakati zoezi litakapoanza katika Jimbo la Madaba watu wajitokeze kwa wingi”.
Hata hivyo Mohamed ametoa rai kwa viongozi wa dini kuhakikisha wanawahamasisha waumi katika kushiriki zoezi hilo.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 15,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa