Wananchi wa kijiji cha Ifinga kata ya Matumbi Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamemshukuru serikali kwa kuboresha barabara ya Ifinga yenye urefu wa kilometa 48 kutoka barabara kuu ya Songea-Njombe ambapo hivi Sasa wanatumika saa moja badala ya saa 16.Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ifinga Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma Komred Odo Mwisho amesema serikali inatekeleza miradi mbalimbali katika kijiji hicho ikiwemo Uboreshaji wa barabara,miundombinu ya shule ya Msingi,sekondari na afya Kata ya Matumbi ina kijiji kimoja kinachoitwa Ifinga hata hivyo serikali inatekeleza miradi mbalimbali kama ilivyo katika kata nyingine zenye vijiji vingi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Teofanes Mlelwa amewaagiza waheshimiwa madiwani wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia miradi yote ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na serikali Katika kata zao.Mheshimiwa Mlelwa alikuwa anazungumza kwenye mkutano wa Baraza la madiwani la Halmashauri hiyo mjini Madaba
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa