Paroko katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mahanje Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Titus Raphael ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ugawaji wa miche bure itakayosaidia utunzaji wa Mazingira.
Hayo amesema mara baada ya zoezi la ugawaji wa Miti lililofanyika katika Kata ya Wino amesema zoezi hilo la ugawaji wa miti linaenda kutunza mazingira.
“Maaskofu mwaka jana walikuwa na mkutano wa kutunza mazingira na kuhimiza wananchi watunze mazingira ili mazingira yaweze kukutunza pia kwa kuweza kupata hali ya hewa nzuri na mvua za kutosha “.
Raphael amesema zoezi la upandaji miti linahitaji umakini ili liweze kutusaidia kupata mazingira rafik na mvua ya kutosha ikiwa katika maeneo mengi yamekuwa hayana mvua za kutosha kutoka na kukosa miti ya kutosha.
Hata hivyo Paroko ameipongeza Serikali kwa kufanya jitihada ya kuhakikisha Viwanda vinajengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba utakuwa uzalishaji utakaopelekea wananchi kupata fedha za kujikimu.
“Tunaiomba Serikali iweze kututimizia jambo hili kwa uharaka kwa sababu tunamiti mingi ambayo inakaria kuvunwa kiwanda kikiharakishwa kujengwa kitasaidia watu wengi kujipatia fursa “.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 16,2025.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa