MKuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema hajaridhishwa na Usimamizi wa miradi ya BOOST na SWASH Halmashauri ya Madaba hali iliyosababisha miradi hiyo kutokamilika na kutekelezwa chini ya kiwango.Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo katika kijiji cha Lipupuma Kanali Thomas amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba,Mkuu wa Wilaya ya Songea na Kamati za Usimamizi wa miradi kusimamia kwa nguvu zote ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa kuwa muda wa utekelezaji umekwisha na wanafunzi wanatakiwa kuanza kutumia miundombinu hiyo.Miradi ya BOOST iliyokaguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika Halmashauri ya Madaba ni ujenzi wa madarasa mawili na vyoo shule ya Msingi Ngembambili unaotekelezwa kwa zaidi ya milioni 52,mradi wa ujenzi shule mpya ya msingi Lipupuma unaogharimu shilingi milioni 331 na mradi wa ujenzi wa vyoo matundu 13 katika shule ya msingi Sokoine kijiji cha Ngadinda unaogharimu shilingi milioni 34
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Teofanes Mlelwa amewasisitiza Waheshimiwa Madiwani Kusimamia Miradi ya Boost.
Hayo ameyasema katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu ya mwaka 2022/2023.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri Mwenyekiti amesema Waheshimiwa Madiwani wasimamie miradi ya Boost inayojumuisha ujenzi wa Madarasa ya Shule za Msingi na Awali na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa