WATUMISHI wa Ifinga Kata ya Matumbi Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma walikuwa wanatumia nusu ya mshahara wao kwa safari pia wananchi walikuwa wanakodi pikipiki kwa shilingi 15,000 hadi eneo lenye mtandao wa simu ili kupiga simu,Akitoa historia ya kijiji cha Ifinga Kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amesema kijiji hicho tangu uhuru kilikuwa na changamoto nyingi ambazo sasa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imezipatia ufumbuzi wa kudumu.Amezitaja changamoto ambazo tayari zimetatuliwa kuwa ni matengenezo ya barabara,kuweka huduma ya Mawasiliano ya simu.kuweka huduma ya maji ya bomba na kuanza mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya.Ifinga ni kijiji pekee mkoani Ruvuma ambacho kipo kilometa 48 toka barabara kuu ya Songea-Njombe ambacho kinaunda Kata ya Matumbi yenye kijiji kimoja cha Ifinga.
Rais samia ametoa shilingi milioni 200 kwa mwaka huu wa fedha 22/23 za ujenzi wa madara 10 katika Halmashauri ya Madaba
Mkoa wa Ruvuma umeingia mikataba 13 na wakandarasi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni sita kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali za matengenezo ya barabara na ujenzi wa madaraja na makaravati.Mgeni rasmi katika hafla ya kuingia mikataba hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Wahabu Nyamzungu amesema mikataba hiyo ni utekelezaji wa hatua ya pili kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA Mkoa wa Ruvuma una mtandao wa kilometa 7146.22 ya mtandao mzima.
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa