Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu (2 in 1) katika Shule ya Sekondari Lilondo, iliyopo Kata ya Wino, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma, umekamilika kwa asilimia 100%. Mradi huu umegharimu jumla ya Shilingi Milioni 95.
Nyumba hii ya walimu aina ya 2 in 1 ina vyumba viwili vya kuishi ambavyo vimeunganishwa katika jengo moja, kila kimoja kikiwa na sehemu ya sebule, jiko, choo na bafu. Lengo kuu la mradi huu ni kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu wa shule hiyo kwa kuwapatia makazi bora, ya karibu na shule, ili kuongeza ufanisi katika ufundishaji na utoaji wa elimu kwa wanafunzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Sajidu Idrisa Mohamed, ameongoza timu ya wataalamu kutembelea eneo la mradi na amempongeza Mwalimu Mkuu kwa usimamizi mzuri wa kazi hii muhimu kwa maendeleo ya elimu, Aidha amewasihi walimu kwa ujumla kutunza mazingira ya shule hiyo ili yaendelee kuwa salama, safi na rafiki kwa wanafunzi na walimu.
Utekelezaji wa mradi huu ni sehemu ya jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha sekta ya elimu kupitia uboreshaji wa miundombinu, hasa vijijini, ambapo changamoto ya makazi kwa walimu imekuwa kubwa. Kukamilika kwa nyumba hii ni hatua muhimu katika kuongeza motisha kwa walimu na kuvutia walimu waliobobea kufanya kazi katika maeneo ya vijijini.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa