Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Wakili Sajidu Idrisa Mohamed, ametoa pongezi maalum kwa Mkuu wa Idara ya Kilimo na timu yake kwa kufanikisha ushiriki wenye mafanikio makubwa katika Maonesho ya Nane Nane Mkoa mwaka 2025.
Mkurugenzi amesema ushindi wa Mshindi wa Kwanza wa Halmashauri ya Madaba kwa Mkoa wa Ruvuma na Mshindi wa Tatu wa Jumla uliopatikana ni kielelezo cha juhudi, mshikamano, ubunifu na kujituma bila kuchoka kwa timu hiyo.
"Kufanikisha ushindi wa Mshindi wa Kwanza na Mshindi wa Tatu wa Jumla ni ushahidi wa juhudi, ubunifu, mshikamano, na kujituma kwenu bila kuchoka. Mmeendelea kuiletea heshima kubwa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na kuonesha mfano bora wa utendaji wa kazi wenye tija," amesema Wakili Sajidu katika salamu zake za pongezi.
Aidha, amewahimiza kuendeleza mshikamano na bidii ya kazi ili kuendelea kufanikisha malengo ya maendeleo kwa wananchi wa Madaba.
Maonesho ya Nane Nane mwaka 2025 yamewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, yakilenga kuhamasisha ubunifu na mbinu bora za kuongeza tija katika uzalishaji.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa