Meneja wa Kilimo wa Kampuni ya AVIV, akiwa ameambatana na wataalam mbalimbali, ametembelea Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji, Wakili Sajidu Idrisa Mohamed pamoja na Mkuu wa Idara ya Kilimo.
Mazungumzo hayo yamelenga kujadili mpango wa kampuni hiyo kuwekeza katika kilimo cha kahawa ndani ya Halmashauri ya Madaba, ikiwemo pia kuwekeza katika ununuzi wa kahawa inayozalishwa katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hii.
Uwekezaji huo unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Madaba, ikiwa ni pamoja na fursa za ajira, upatikanaji wa miche bora ya kahawa kwa wakulima, na uboreshaji wa huduma za kijamii kama vile afya na elimu.
Halmashauri ya Madaba ipo tayari kushirikiana na kampuni hiyo ili kuhakikisha uwekezaji huo unatekelezwa kwa manufaa ya wananchi na maendeleo ya sekta ya kilimo hususan kahawa.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa