• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

Posted on: June 19th, 2025

Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imepongezwa rasmi kwa kupata hati safi katika Ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/2024, hatua inayodhihirisha uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali za umma.

Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 19 Juni, 2025, na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi Marry Makondo, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed, wakati wa mkutano maalum wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.

Katika hotuba yake, Bi Makondo aliwapongeza viongozi na watendaji wa Halmashauri kwa kazi nzuri iliyopelekea kupata hati safi. Alisema:

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Ndg. Sajidu Idrisa Mohamed, akiwasilisha taarifa ya CAG, alieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na utekelezaji wa hoja na maagizo ya ukaguzi kwa ufanisi, hali inayoonyesha dhamira ya Halmashauri katika kusimamia fedha za umma kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Mhe. Teofanes Mlelwa, aliwashukuru madiwani na wataalamu kwa ushirikiano na juhudi zao ambazo zimeiwezesha Halmashauri kupata hati safi kwa kipindi chote cha uongozi wao.

Kupatikana kwa hati safi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ni ishara ya mafanikio makubwa ya kiutawala, na ni chachu kwa Halmashauri kuendelea kuimarisha misingi ya uwazi, uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali za umma kwa maendeleo ya wananchi wa Madaba.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UHISHWAJI WA BARAZA LA WAZEE MADABA WAFANYIKA LITUTA.

    November 22, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPEWA CHETI CHA PONGEZI KWA UTEKELEZAJI BORA WA LISHE

    November 21, 2025
  • TIMU YA UKAGUZI MKOA WA RUVUMA YAFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MADABA.

    November 08, 2025
  • TIMU YA UKAGUZI KUTOKA MKOANI YATUA MADABA KWA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO.

    November 06, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa