Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamefanikiwa katika zoezi la umezeshaji wa dawa katika ngazi ya shule na jamii kwa magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele mwaka 2024 watu 55,707 sawa na asilimia 89.
Akitoa taarifa hiyo mratibu wa magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele Waziri Ramadhan katika kikao cha mapitio na mpango mkakati wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele amesema mpango huo ulifanikiwa kwa watu 55707 walimeza dawa kati ya watu 62,922 walioandikishwamwaka 2024.
Amesema mwaka 2024 halmashauri ya Wilaya ya Madaba ilipokea zaidi ya shilingi Milioni 87 ambazo zilitumika katika zoezi la ugawaji wa dawa katika ngazi ya shule na Jamii.
Hata hivyo amesema mafanikio ya zoezi la umezeshaji wa dawa ikiwemo kufahamu umuhimu wa kuzingatia kinga tiba zinazotolewa ,tumegawa za usubi katika ngazi ya jamii kwa zaidi ya asilimia 80.
“Tumeweza kupunguza kiasi cha wagonjwa wanaoripoti katika vituo vya kutolea kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na tumemezesha dawa ya minyoo ya tumbo na kichocho ngazi ya shule na kwa zaidi ya asilimia 99.5”
Ramadhani amesema mwaka 2025 zoezi litafanyika Januari 21 hadi 22 kwa ngazi ya shule na kutarajia kutoa dawa kwa jumla ya wanafunzi 13,574.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 15,2025
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa