Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile ameambatana na Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Madaba,wataalam,na wenyeviti wa Vijiji wametembelea na kujifunza katika Kiwanda cha Lush chanzo wood kinachotengeneza mbao pana kwakutumia magogo ya miti.
Msimamizi wa Kiwanda hicho Justin Mligo akizungumza katika ziara hiyo amesema magogo hayo yakibadilishwa kuwa mbao pana zinatengenezewa samani kama vile meza,viti,makabati na kadhalika.
Mligo amesema mbao hizo wanaziuza katika Nchi ya Mikoa mbalimbali Nchini Tanzania pamoja na Nchi za Nje.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Teofanes Mlelwa akitoa shukrani ya kupewa elimu ya kutumia magogo ya miti yanayobaki baada ya kuvuna miti na kubadilisha kuwa mbao pana amesema kuwa wamejifunza vitu vingi katika Kiwanda hicho ikiwa mazao ya miti ya Madaba yanaweza kuzalisha mbao kama hizo na kutengeneza samani mbalimbali.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa