Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela mwampamaba ametoa rai kwa awananchi kuwa na subira katika suala la mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri.
Hayo amesema katika mkutano wa baraza la Madiwani la robo ya kwanza Julai Septemba 2024/2025 lililofanyika Novemba 20,2024.
“Mikopo yetu ya asilimia 10 iko wazi siyo mikopo ya siri wananchi naomba mjue kuwa haiwezekani mikopo hii ikatolewa kwa wakati mmoja kwa watu wote hata kama unavigezo vya kuweza kupata mikopo naomba muwe na subira”.
Hata hivyo amesema mikopo hiyo ya asilimia 10 itatolewa kwa awamu kwa kila kikundi na kunufaika na mikopo hiyo ya asilimia 10.
“Naomba sana ndugu zangu mnaohusika na kutoa elimu kuhusu mikopo hii tuwaelimishe wananchi kwamba itatolewa kwa uwazi na haichangishwi pesa ya aina yoyote tumeona baadhi ya amaeneo watu wanalalamika wanataka watu wote wapate kwa wakati mmoja uwezo huo serikali haina”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 20,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa