Afisa Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma Amandus Chilumba ametoa rai kwa Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara kuendelea kuta elimu na kuwasisistiza kujitokeza siku ya uchaguzi Novemba 27,2024.
Hayo amesema katika mkutano wa Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ikiwa katika zoezi la uandikishaji halmashauri ya Wilaya ya Madaba ilifanya kwa asilimia 105.0.
“Mheshimiwa Mwenyekiti kipindi cha kuandikisha Madaba tulifanya kwa asilimia 105.0 na katika kipindi cha kupiga kura tukirudi nyuma kazi yetu itakuwa haijakamilika kwa asilimia miamoja.
Hata hivyo amesema kupitia Baraza hilo tukufu amewaomba Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara kuendelea kutoa elimu ili siku ya uchaguzi Novemba 27,2024 wananchi wajitokeze kwa Wingi kuchagua viongozi walio bora ambao wataweza kuongoza.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 20,2024
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa