Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amesema Serikali ya awamu ya sita imeendelea kutoa Mbolea za Ruzuku katika sekta ya kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Hayo amesema katika Mkutano wa Baraza la Madiwani kuwa katika kuendelea kutoa Mbolea za Ruzuku Serikali zinaendelea kutoa mikataba katika kampuni ili waweze kuwahudumia wananchi.
“Niombe tuendelee kufuatilia katika maeneo yetu na pale ambapo itatokea kunachangamoto tunao maafisa ugani wetu katika maeneo hayo watatua changamoto hizo”.
Mkurugenzi amesema Mbolea za Ruzuku inaendelea kutolewa kwa wakulima ambao wamesajiliwa katika mfumo ikiwa halmashauri ya Wilaya ya Madaba imezalisha tani 17,232 mwaka 2024.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Novemba 20,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa