HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba imepokea zaidi ya shilingi Bilioni 8 kutoka Serikali kuu kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Elimu Msingi Elimu Sekondari ,Afya na Utawala.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed kuwa kwa kipindi cha Mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2023/2024 Halmashauri imetekeleza Miradi mbalimbali na kukamilika kwa asilimia 100.
Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia imewasikia na imewafikia wananchi kwa kutoa kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 1 kupitia divisheni ya Elimu Msingi,kwaajili ya ujenzi wa vyumba 39 vya madarasa na matundu 144 ya vyoo.
Hata hivyo amesema wamefanikiwa kukamilisha chumba kimoja cha darasa ukarabati wa shule Kongwe 4 ujenzi wa hosteli moja ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu na ujenzi wa nyumba 4 za walimu katika divisheni ya Elimu Msingi.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 8,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa