Kikao cha Lishe kilichofanyika Halmashauri ya Wilaya ya madaba, Novemba 25, 2025 kikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Kapenjama Ndile, ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho. Washiriki kutoka sekta mbalimbali walijadili kwa kina hali ya lishe wilayani na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha ustawi wa wananchi, hususan watoto.
Katika taarifa ya utekelezaji, imebainishwa kuwa utoaji wa Vitamin A umefikia asilimia 97.7, huku utoaji wa vidonge vya kuongeza damu kwa kinamama ukifikia takribani asilimia 99.9. Aidha, mpango wa chakula shuleni unaendelea kutekelezwa katika shule 10, ambapo tayari tani 10 za chakula zimepokelewa na kusambazwa.
Kwa upande wa tathmini ya hali ya lishe, watoto 24 kati ya 599 wamegundulika kuwa na uzito pungufu, sawa na asilimia 4.01. Wajawazito wenye upungufu wa damu wamefikia asilimia 16 Kati ya 714 waliofanyiwa vipimo sawa na 2.2%, watoto 11 kati ya 4,517 wameonekana kuwa na udumavu, sawa na asilimia 0.2. Na watoto 3 Kati ya 4517 wamekutwa na uzito uliokithiri
Mkuu wa Wilaya alitoa maelekezo mahsusi kuhakikisha changamoto za lishe zinapungua na huduma zinaboreshwa. Alisisitiza kuwa watoto wanaobainika kuwa na uzito pungufu wahakikiwe kwa kina ili kubaini chanzo cha tatizo, ikiwa ni pamoja na kubaini kama linatokana na maradhi au changamoto za upatikanaji wa chakula. Aidha, alitaka taarifa za upimaji wa lishe zilinganishwe na misimu ili kubaini kama mabadiliko ya upatikanaji wa chakula yanachangia matatizo yanayoonekana.
Vilevile, aliagiza kila shule kuhakikisha inazalisha angalau tani mbili za chakula kwa mwezi ili kuimarisha mpango wa chakula mashuleni. Pia alisisitiza kuwa ugawaji wa maharage aina ya jeska kwa shule uanze mara moja ili kuongeza upatikanaji wa chakula chenye virutubisho na kuboresha lishe ya wanafunzi.
Katika hitimisho, Mkuu wa Wilaya alisisitiza kuwa utekelezaji wa hatua hizo unahitaji ushirikiano kutoka sekta zote. Alisema kuwa kuboresha lishe ni jukumu la kila mmoja kwa kuwa “lishe bora ndiyo msingi wa afya, uwezo wa kujifunza na nguvu kazi ya taifa.”
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa