• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

WATAALAMU WA AFYA NGAZI YA MSINGI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA WAANZA MAFUNZO MAALUM YA KUBORESHA HUDUMA KWA WAZEE

Posted on: November 26th, 2025

Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imezindua mafunzo ya siku tatu kwa Wataalamu wa Afya ngazi ya msingi, yakilenga kuboresha huduma za kinga, utambuzi na ufuatiliaji wa magonjwa ya wazee, magonjwa yasiyoambukiza, afya ya uzazi pamoja na huduma za wagonjwa majumbani. Mafunzo haya yanafanyika kuanzia tarehe 26–28 Novemba 2025 kwa ushirikiano kati ya Shirika la PADI na HelpAge Tanzania, na yanajumuisha wataalamu kutoka vituo mbalimbali ndani ya Halmashauri.


Akizindua mafunzo hayo, Mganga Mkuu wa Halmashauri, Dkt. Mussa Rashid, alisisitiza umuhimu wa kuwaandaa wataalamu wa afya kukabiliana na changamoto za wazee, ikiwemo udhaifu wa mwili, kupungua kwa kumbukumbu, na kuongezeka kwa magonjwa kama shinikizo la damu na kisukari.


Dkt. Rashid aliwataka washiriki kuzingatia maadili ya kazi na nidhamu wakati wote wa mafunzo, huku wakihakikisha wanatoa elimu ya kinga kwa jamii kuhusu magonjwa ya mlipuko na umuhimu wa usafi wa mazingira. Pia aliwakumbusha kuendeleza ujumbe wa kuimarisha amani katika maeneo yao ya kazi kama sehemu ya msingi ya ustawi wa wananchi.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuhamasisha wazee kufanya mazoezi kulingana na mazingira na tamaduni za eneo husika, ikiwemo kushiriki ngoma za asili, kutembea na kufanya mazoezi mepesi yanayosaidia kuimarisha afya ya mwili na akili. Mazoezi haya ni sehemu muhimu ya kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza na kuongeza ubora wa maisha ya wazee.

Mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza uwezo na ujuzi wa wataalamu wa afya katika kutoa huduma bora kwa wazee na kuboresha huduma za NCDs, SRH na HBCs, hivyo kuiwezesha Halmashauri ya Madaba kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika utoaji wa huduma za afya kwa makundi maalum.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • WAHITIMU WA UFUNDI STADI KUPATIWA VIFAA VYA KUANZIA KAZI VYENYE THAMANI YA MILIONI 4.4

    November 27, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA NGAZI YA MSINGI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA WAANZA MAFUNZO MAALUM YA KUBORESHA HUDUMA KWA WAZEE

    November 26, 2025
  • DC NDILE ATOA MAELEKEZO YA KUIMARISHA AFUA ZA LISHE MADABA

    November 25, 2025
  • UHISHWAJI WA BARAZA LA WAZEE MADABA WAFANYIKA LITUTA.

    November 22, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa