HALMSHAURI ya Wilaya ya Madaba kwa kipindi cha mwaka wa Fedha 2021/2022 hadi 2023/2024 Serikali ya awamu ya Sita imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 2 Kwaajili ya uteekelezaji wa Miradi ya maendeleo divisheni ya Elimu Sekondari.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed ofisini kwake kuwa Elimu Sekondari wametekeleza ujenzi wa vyumba 46 vya madarasa,ukamilishaji wa maabara na ujenzi wa Shule mpya 2,ujenzi wa nyumba 3 za walimu,ukamilishaji wa hosteli,ukamilishaji wa bwalo na ujenzi wa nyumba 5 za walimu.
Hata hivyo amesema utekelezaji wa Elimu bila malipo Serikali imeendelea kutoa Sera ya utoaji wa Elimu bila malipo kwa mafanikio ambapo kwa kipindi cha 2021/2022 hadi kufikia Novemba 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imeendelea kupokea fedha kiasi cha zaidi ya shilindi Milioni 426 kutoka Serikali kuu.
Amesema Serikali ya awamu ya sita imewasikia na imewafikia wananchi kwa kusaidia upatikanaji wa magari 2 kwaajili ya shughuli za usimamizi wa utoaji na uendeshaji wa elimu kwa Divisheni ya Elimu Msingi na Sekondari yamegharimu Milioni 190.
“Halmshauri inaendelea kufuatilia na kutekeleza kwa ufanisi utoaji wa Elimu bila malipo ili fedha ya Serikali inayowekezwa iweze kutoa matokeo chanya katika kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika Mitihani ikiwemo kuimarisha taaluma na elimu kwa ujumla.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba,
Januari 8,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa