Timu ya Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Joel M. Mbewa imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba leo tarehe 06 Novemba 2025.
Katika ziara hiyo, timu ilitembelea miradi kadhaa ikiwemo ujenzi wa nyumba nne za walimu katika Shule ya Sekondari Matetereka, mradi uliogharimu shilingi milioni 201.9 kwa ufadhili wa Wakala wa Elimu Tanzania (TEA). Nyumba hizo zimekamilika na zimeanza kutumika rasmi.
Aidha, timu ilikagua mradi wa kituo cha walimu Ifugwa unaogharimu shilingi milioni 51.4, ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 20 Novemba 2025, pamoja na mradi wa Barrick Sekondari Madaba unaojumuisha ujenzi wa madarasa sita, mabweni mawili na vyoo 12, ambao uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji. Pia, walitembelea mradi wa Stendi ya Madaba unaotekelezwa kwa ufadhili wa TASAF kwa gharama ya shilingi milioni 205.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mbewa alisisitiza umuhimu wa miradi kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, huku akiwataka wasimamizi wa miradi kuendelea kuwahimiza mafundi kuhakikisha kazi inafanyika kwa viwango vinavyostahili. Katika miradi iliyokamilika, hususan nyumba za walimu, aliwasisitiza watumiaji kutunza miundombinu hiyo ili idumu kwa muda mrefu.
Ziara hiyo inaendelea leo kwa ukaguzi wa miradi mingine inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Madaba.


MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa