ZAIDI ya Hekta 500 za Mashamba ya Miti ya Wananchi Wino Halmashauri ya Wilaya ya Madaba yameteketea kwa moto na kujeruhi watu wanne waliokuwa wakizima moto huo.
Afisa wa Shamba la Miti Wino Geofrey Shio amesema moto huo umetokea Oktoba 11 ,2023 ikiwa chanzo cha moto huo mwananchi mmoja alikuwa anapika chakula katika eneo hilo na moto kupeperuka na kuteketeza mashamba ya miti.
Shio amesema Shamba la Serikali la Wakala wa Misitu Wino TFS limeaungua kwa sehemu ndogo asilimia 0.3
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amefika katika eneo hilo ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanadhibiti moto na kuendelea kulinda miti iliyopandwa.
“Halmshauri ya Madaba tunategemea uchumi wa misitu kwa miaka ijayo tunawasihi wananchi waliende mazingira na kuhakikisha hautokei uzembe ambao utaharibu rasilimali zetu za Misitu”.
Mkurugenzi amesema Halmashauri ya Madaba katika eneo hilo kuna wawekezaji wengi ambao wamewekeza katika kilimo cha Miti kwa hekta nyingi.
“Mwaka jana tulipa changamoto katika mashamba ya TFS hekta nyingi ziliungua tuhakikishe sisi sote kwa pamoja tunaungana ili tuweze kutunza rasilimali za uchumi wetu wa baadae”.
Hata hivyo Mkurugenzi ametoa pole kwa uongozi wa TFS kwa vijana waliopata majeraha ya kuungua moto ambao watatu wapo Hospitali ya Peramiho na mmoja yupo kituo cha Afya Madaba.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Oktoba 12,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa