Halmashauri ya Madaba wameanza utekelezaji wa mradi wa Boost unaotekelezwa kwa zaidi ya shilingi Milioni 600 katika mwaka wa fedha 2022/2023.
Timu ya wataalamu wa Halamshauri hiyo imetembelea Kata ya Mahanje ambayo katika mradi huo wamepewa Shule 2 ya Mahanje na Ifugwa.
Afisa Elimu Msingi Vifaa na takwimu Raphael Kibiligi wa Halmashauri hiyo amesema kwa awamu ya kwanza ya mradi wamepewa shule 6 kati ya shule 28 timu hiyo yenye wataalamu 12 imeanza kutamburisha mradi kwa wananchi wa Kata ya Mahanje.
Hata hivyo amesema Shule ya Msingi Mahanje imepewa ujenzi wa vyumba 2 vya Madarasa yenye thamani ya shilingi Milioni 48,000,000/= na matundu ya vyoo 3 yenye thamani ya Shilingi milioni 5,100,000/= jumla katika Shule hiyo Milioni 53,100,000/=.
Katika Shule ya Msingi Ifugwa wamepewa zaidi ya shilingi milioni 66 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 2 ya awali ya mfano na matundu ya vyoo 6 ikiwa vyoo 2 vya walemavu na vyoo vinne vya kawaida.
Kaimu Mwenyekiti wa timu hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii Bashiru Mgwasa akizungumza na hadhara katika Kata ya Mahanje amesema majukumu ya wananchi ikiwa ni pamoja na kutambua mradi na fedha zilitengwa kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya Shule,Kuandaa eneo la ujenzi na kuhakikisha eneo hilo halina migogoro.
Amesema wananchi wajibu wao ni pamoja na kuchimba mashimo ya vyoo,kusafisha eneo la ujenzi pamoja na kuchimba msingi wakati wa ujenzi.
Diwani wa Kata ya Mahanje Stephano Mahundi akizungumza na wananchi hao ametoa rai kwa wananchi hao kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo kwa weledi na kutoa taarifa kwa viongozi kwa wale watakaoenda kinyume na matakwa ya Serikali.
“Mradi huu umekuja kwaajili ya sisi wanamahanje naomba kwa vile umekuja kwetu haijawahi kutokea darasa kujengwa kwa shilingi milioni 24 na Madarasa haya ya mfano tuhakikishe tunasimamia kwa nidhamu ya hali ya juu sana”.
Hivyo Mahundi amewasihi wananchi kuwa na umoja mara baada watakapoambiwa kusafisha eneo,kuchimba msingi baada ya hapo utaratibu utaendelea kwaajili ya ujenzi na kuhakikisha usimamizi wa ujenzi huo upo mikononi mwa wananchi.
Kutoka Halmashauri ya Madaba
Aprili 24,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa