KATIBU Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile katika kikao cha Wilaya ya Songea cha kutoa maoni ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2026/2050.
Mwampamba akizungumza katika kikao hicho amesema mwaka 1961 mara baada ya kupata uhuru Nchi ya Tanzania ilikuwa inaongzwa na ujamaa na mara baada ya kufika mwaka 1980 ikaonyesha kuwa Watanzania wanatakiwa kuwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo.
“Mambo mengi ambayo tuliyokuwa tunafanya kama ujamaa au ushirika tukaona hauwezi kuendena na ulimwengu wa sasa tayari teknolojia ilikuwa imebadilika na ilipofika mwaka 1986 tuliunda dira yetu ambayo iljikita katika kuhamasisha amani, utulivu,umuhimu wa kufanya kazi, na umuhimu wa kuwa wazalendo katika Taifa letu ilienda mpaka mwaka 1999”.
Katibu Tawala amesema mwaka 2000 aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamini Mkapa aliasisi dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2000 hadi 2025 ambayo inatumika mpaka sasa.
“Aliasisi kwasababu teknolojia ilikuwa imekuwa sana duniani tusingeweza kuishi kama kuwa na kuendelea ya kilimo kisicho na tija,ujamaa ambao umekufa ,kuhozi viwanda vyetu Mkapa aliamua kubadilisha mfumo huo na kuingia kwenye mfumo wa utandawazi”.
Hata hivyo amesema serikali iliweza kumiliki uchumi na kuwa na miundo mbinu mizuri ya barabara,afya,elimu na kuweza kuwa na uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuwa na amani na usalama wanchi ya Tanzania.
“Dira yetu ya mwaka 2000 hadi 2025 inaisha mwaka kesho tunahitaji kuwa na dira ya mwaka 2026 hadi 2050 pamoja na mabadiliko makubwa ambayo Taifa limepitia bado tumepata changamoto za ajira elimu haiwezi kumfanya mtoto kujiari kwa sababau wengi wanaufaulu wa kwenye makaratasi”.
Kutoka kitengo cha mawsiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 12,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa