WILAYA ya Songea wamefanya Kikao cha kamati ya ushauri cha Wilaya (DCC) wakijumuisha Halmashauri tatu Manispaa,Songea Vijijini na Halmashauri ya Madaba.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile akizungumza katika kikao hicho amezungumzia uchumi wa madini katika Mkoa wa Ruvuma.
“Ipo haja ya kupata andiko la mchango ,na jinsi uchumi huo utakavyogusa wananchi wengine”
Hata hivyo Kamenjama amezungumzia suala la mazingira ya misitu ikiwa Wilaya ya Namtumbo mwaka 2024 wanakaribia kupata Bilioni 4 kupitia misitu kwa kuvuna hewa okaa.
Amesema ili waweze kuboresha uchumi lazima waandae mikutano katika sekta ya madini,misitu na mazao yake ili kuweza kujua Wilaya ya Songea inamisitu kiasi gani na inawanufaisha wananchi kwa kiasi gani.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba.
Januari 19,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa