• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

WAZIRI wa Maji awaomba wakuu wa Mikoa kusimamia miradi ya maji

Posted on: July 6th, 2021

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewaomba Wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa kushirikiana katika usimamizi wa miradi ya maji nchini.


Mhe. Aweso amesema hayo katika kikao cha mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanzania Bara kinachofanyika jijini Dodoma.


Amesema Wizara ya Maji imedhamiria kuhakikisha lengo la kumtua mama ndoo ya maji linafikiwa kama lilivyoelekezwa na serikali.

"Niwaombe viongozi tushirikiane kwa dhati kuhakikisha tunaondoa changamoto zote za upatikanaji wa huduma ya majisafi. Peke yetu hatutaweza." Aweso amesema.


Pamoja na hilo amepokea mapendekezo mbalimbali kutoka kwa viongozi hao wa mikoa na kuwaahidi kuyafanyia kazi.


“Kuhusu kuwa na utaratibu wa wadau wa maji kukutana na kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na sekta ya maji ni jema sana.

Naomba nipokee ushauri wenu wa jinsi ya kulitekeleza ili liwe endelevu. Isiwe ni maelekezo ambayo yanaweza kubadilishwa na kiongozi mwingine. Liwe ni muongozo rasmi na utamaduni ili hata kiongozi ajaye, afanye hivyohivyo" Aweso amesema.


Amesisitiza kuwa Wizara ya Maji haitakuwa kikwazo katika kufikia malengo. Amezitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Wizara ili kuimarisha usimamizi wa miradi ya maji kuwa ni pamoja na uamuzi wa kuingia makubaliano na Chuo cha Maji ili kuwatumia wahitimu wa chuo hicho katika usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji nchini.


Wakuu hao wa mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanzania Bara wanashiriki mafunzo ya uongozi Jijini Dodoma.

Imeandikwa na Afisa Habari Wizara ya Maji Dodoma

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa