Wawekezaji wa Kampuni ya Xiwang kutoka Nchi ya China wamepewa shamba lenye Hekari 10,000 lililopo Kijiji cha Ngadinda Kata ya Gumbiro Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwaajili uwekezaji wa kilimo cha mifugo.
Akizungumza Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama amesema shamba hilo la Serikali lilikuwa na hekari 15,000 ambapo hekari 5000 wamepewa wananchi kwaajili ya kilimo na wawekezaji wamepewa hekari 10,000 kwaajili ya uzalishaji wa vyakulia vya mifugo
“Wananchi mmepewa hekari 5000 na eneo lililobaki tunampa mwekezaji kwaajili ya kilimo na siyo ufugaji bali ni kilimo cha mahindi ya njano soya na huu ndio mkakati wetu naomba tutoe ushirikiano shamba siyo letu ni la Wizara”.
Meneja wa Kampuni hiyo Savio Chanahi amesema wamejipanga kwaajili ya uzalishaji wa mahindi ya njano na soya na ufuta na watakuwa wanabadilisha mazao kwa kurutubisha ardhi na kulinda mazingira.
“ Sisi tumejipanga mara tu Wizara itakapo tukabidhi Shamba tumejipa miezi miwili mtaanza kuona vifaa kwaajili ya matumizi ya kilimo”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Februari 17,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa