MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amekemea tabia za watumishi wanaopenda kuwazushia wengine mambo mabaya kwa viongozi.
Hayo ameyasema katika Sikukuu za Mei Mosi zilizofanyika Manispaa ya Songea Viwanja vya Majimaji na kuhudhuria viongozi mbalimbali na watumishi kutoka katika Halmashauri zote 8.
Amesema watumishi wote wanayonafasi kubwa kufanya kazi katika Serikali ya awamu ya sita wapo watanzania wengi wenye sifa,hivyo nafasi mliyopewa ya kusukuma maeendeleo katika Taifa la Tanzania.
“Hivyo kumekuwa na taarifa nyingi ambayo ninyi kama familia ya wafanya kazi mmekuwa na tabia ya kutafutiana na kuzushiana, kuwasemea wenzenu kwa mambo ambayo hawayatendi”.
Hivyo Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa watumishi wote kuhakikisha wanapendana ikiwa wote ni familia moja ambayo wanajenga nyumba moja kwa nia ya kuwasaidia wananchi wa Tanzanaia pamoja na kumasaidia Rais wa Tananzani.
“Hivyo niwaombe acheni tabia hizo ambazo zinasababisha wengine wanaofanya kazi kwa bidii kukata tamaa,tuache yaliyopita tugange yajayo”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa