HALMASHAURI ya Madaba Wilaya ya Songea imeadhimisha Muungano wa miaka 58 kwa kufanya Usafi wa Mazingira maeneo ya Kituo cha Afya.
Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed mara baada ya zoezi hilo amesema Sikukuu hiyo itaendelea kuwa alama ya mafanikio ya Muungano katika nchi ya Tanzania na Zanzibar pamoja na kuwaenzi Viongozi ambao ndio waasisi wa Taifa la Tanzania.
“Tudumishe Muungano kama ambavyo tulivyojumuika kwa pamoja sisi wananchi wa Halmashauri ya Madaba kwa kuunga Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani,tukishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuhimiza wananchi kuweka mazingira katika hali ya Usafi”.
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Mussa Rashid amewapongeza wanafunzi kutoka Shule ya Madaba Day pamoja na Mahanje kwa kusherekea sikukuu ya Muungano kwa kuweka Mazingira safi na kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Na hii inaonyesha kwa jinsi gani tunavyomuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan,leo ni siku muhimu katika Taifa letu na tunawaenzi viongozi wasisi wa Taifa letu Nchi imekuwa na Umoja”.
Hata hivyo Mganga Mkuu amewasa Wanafunzi hao kuendelea kuwa wazalendo kupitia kazi kubwa waliyofanya leo kwa kuweka mazingira katika hali ya usafi na hata watakapokuwa watumishi mara baada ya kuhitimu masomo yao wakaendelee kuwa na moyo wa uzalendo.
“Moyo wa uzalendo usiishie leo tunatarajia kuwaona mnasoma kwa bidii, mkiwa na nidhamu ya hali ya juu na tunatarajia kuwaona mnachapa kazi kwa bidii”.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Madaba Anita Makota amesema katika zoezi hilo la usafi katika siku ya Muungano limekuwa jambo jema kwanza ni mazoezi na kuendeleza kazi pamoja na kuleta maendeleo na mshikamano.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Madaba Day Saimon Emanuel amesema zoezi hilo la kufanya Usafi katika kituo cha afya , kwanza limesaidia kuwaweka kwa pamoja na viongozi wa Halmashauri hiyo pamoja na kuyaenzi yale ambayo viongozi wa Taifa walianzisha.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
April 26,2022
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa