Wataalamu Halmashauri ya Madaba wamepewa mafunzo ya Mfumo wa FFARS kwa kuwajengea uwezo juu ya manunuzi na matumizi ya fedha za Umma.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkurugenzi Mtendhaji wa Halmashauri hiyo Sajidi Idrisa Mohamed amesema mfumo wa FFARS unawakumbusha watendaji wa vijiji na watendaji Kata kwa kuwajengea uwezo kwa matumizi ya Fedha za Serikali.
Mkurugenzi amesema mfumo huo umekuja kwaajili ya kuondoa changamoto na kuepuka hoja za ukaguzi na kufanya malipo kwa kutumia mfumo kwa mfano miradi ya vijiji au miradi ya Serikali zikija kutoka Makao makuu zitakuwa zinaingizwa kwe account za vijiji.
“Nitoe rai kwenu mfumo huu muuelewe na uanze kufanya kazi mwaka wa fedha ujao mtaanza kukaguliwa na wakaguzi wanje na Mkaguzi wa Ndani muanze kwenda kwa utaratibu wa manunuzi na Sheria ya Fedha”.
Mhasibu Msaidizi wa Halamshauri hiyo Dotto Ndeleka amesema imekuwa ni jambo la muhimu sana kwa Watendaji na walimu kupata mafunzo hayo ya mfumo wa FFARS.
Ndeleka amesema kufikia Julai 1, 2023 wanatakiwa kuanza kutumia mfumo huo utapelekea kuweka wazi Matumizi na makusanyo ya Mapato kwa ngazi ya vijiji na Kata.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 7,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa