MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Teofanes Mlelwa amewakabidhi pikipiki 6 watendaji wa Kata.
Akizungumza katika zoezi hilo lililofanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo amempongeza Rais wa awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan kwa kuwaona Watendaji Kata na kuwapa pikipiki ambazo zitarahisisha kutekeleza majukumu yao kwa wakati.
“Sitegemei kuona Mtendaji hajui majukumu yake Rais Samia amewaona kuwa mna kata,vijiji,Mitaa pamoja na vitongoji hivyo mkahakikishe mnatembelea miradi yote ya maendeleo”.
Hata hivyo Mlelwa amewaasa watendaji hao kutumia pikipiki hizo kwa matumizi sahihi na kuepuka kutumia katika mambo yao binafsi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashari hiyo Sajidu Idrisa Mohamed kupitia zoezi hilo amesema watendaji walikuwa wanapata changamoto kwa kutembea kwa umbali wa kilomita 120 kwa kata ya Mtyangimbole na Kata ya Matumbi kilomita 48 kuja Halmashauri wanapohitajika.
“Kupitia hizi pikipiki tulizotoa hatuhitaji kusikia visingizio vya kuchelewesha taarifa na kuripoti miradi inayoendelea katika Kata zenu”.
Hata hivyo Mohamed amesema kutokana na changamoto ambazo zilikuwa zimewapata Watendaji kwa mda mrefu Serikali ya awamu ya Sita imeona uhumimu na kuwapatia pikipiki 6 kwa Kata za Halmashauri ya Madaba ili kuondoa changamoto hizo.
Mohamed ametoa shukrani za dhati kwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaongezea Watendaji ufanisi katika kazi na kurahisisha usafiri katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwataka Watendaji wote wa Kata mliopewa pikipiki hizi kuhakikisha mnazitunza sawa na malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuhakikisha mnazifanyia matengenezo ya mara kwa mara”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Machi 2,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa