HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya mafunzo ya utekeleza wa mradi wa Boost mwaka 2024 /2025.
Katika mafunzo hayo wamehudhuria walimu wakuu sita ambao wamepata mradi watendaji wa vijiji,wahasibu na wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi.
Mratibu wa Boost Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Raphael Kibirigi amesema wamepokea kiasi cha shilingi milioni 398,800,000/= kwaajili ya ujenzi wa matundu 36 ya vyoo na madarasa 12 katika shule sita za msingi.
Mhandisi wa Halmashauri hiyo Ledemta Lweikiza ametoa rai kwa walimu wote ambao wamepata mradi kuzingatia mwongozo wa ujenzi ,vipimo pamoja na kuzingatia maelekezo yote ambayo watapewa na mhadisi katika ujenzi huo.
Naye Afisa Manunuzi Steward Eliak amesema wasimamizi wahakikishe wanakuwa makini katika utekelezaji wa mradi huo kwa kuzingatia bajeti iliyopo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 31,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa