Wastaafu na watumishi waliopo kazini wamepewa semina ya matumizi ya benki ya Azania kwaajili ya kuwekeza akiba na kupata mikopo mbalimbali.
Akizungumza katika semina hiyo Meneja wa tawi la Tunduma Mullaga Sunday amesema benki hiyo inamilikiwa kwaasilimia 99 na mifuko ya jamii kama PSSSF,NSSF,WCF na NHIF na benki ya maendeleo ya Afrika Mashariki.
“Hao wote wanamiliki hisa za benki kwa asilimia 99 na hiyo asilimia moja ni wamiliki wadogo wadogo hii ni benki yetu ya wazawa tuanzie nyumbani”.
Sunday amesema kuwa wanatambua mchango wa wafanyakazi waliopo kazini na hata waliostaafu ikiwa Mkoa wa Ruvuma walifanya semina na wastaafu.
“Mwaka 2018 tulifanya semina na wastaafu Mkoa wa Ruvuma na tulipata wastaafu wengi takribani 400 katika ukumbi wa bomba mbili kwa kutoa mikopo na tulitoa elimu ya fedha maana unaweza kukopa halafu usijue namna ya kutumia”.
Kwa upande wake Afisa wa Azania Mkoa wa Ruvuma Ellen Kabote amesema Azania benki inatoa mikopo kwa mwanamke hodari ambapo anaweza kukopa mara nne ya akiba yake .
“Account yetu ya mwanamke hodari inariba ya asilimia moja tu kama unamilioni moja unaweza kukopa milioni 10 na kama una milioni 10 unakopa milioni 40 lakini vigezo na masharti kuzingatiwa”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 29,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa