Waumini wa kanisa la Wasabato Madaba na wanafunzi wa chuo cha Afya Songea (Songea College ofa health and allied science) wamechangia damu katika hospitali ya Wilaya ya Madaba.
Zoezi hilo limefanyika Disemba 11,2024 jumla ya chupa 19 za damu zimetolewa kwaajili ya uokoaji wa wagonjwa wa dharula, na huduma za mama na mtoto.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mussa Rashid amewapongeza waumini wa kanisa hilo na wanafunzi wa chuo cha Afya Songea kwa kujitoa kutoa damu na kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi wengine.
“Uchangiaji wa damu salama ni hiari na ni muhimu kwa sababu katika hospitali yetu tunauhitaji mkubwa wa damu ili kuokoa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji ikiwa huduma za mama na mtoto zinaendelea,uhitaji wa damu salama ni mkubwa”.
Hata hivyo mratibu wa huduma za maabara ametoa elimu ya uchangiaji wa damu kwa waumini wa kanisa hilo na wanafunzi wa chuo cha afya songea pia ametoa rai kwa wananchi wote kujitokeza kuchangia damu salama ambayo itasaidia kuokoa uhai wa wananchi .
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Desemba 11,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa