HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba leo wamefanya mafunzo ya afua za Lishe kwa Waratibu ngazi ya vituo vya Afya vya Serikali na Visivyo vya kiserikali ya huduma ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamedi akiwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Maternus Ndumbaro amesema waratibu hao kupitia mafunzo hayo wanadhamana kubwa ya kutoa ushauri kupitia mpango shirikishi wa LisheTaifa.
Ndumbaro amesema adhima ya mafunzo hayo katika Halmashauri nikupinga na kutatua hali duni ya Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
“Ndugu waratibu nidhahiri Lishe bora katika jamii nikichocheo cha maendeleo katika Nyanja zote za Afya,Kilimo,Elimu,Biashara na uchumi “.
Hata hivyo amesema jambo la msingi linalotakiwa kuzingatiwa katika Lishe ni suara mtambuka ambapo utapiamlo katika jamii nimatokeo ya matatizo mengi,hivyo umuhimu wa Lishe husaidia maendeleo kwa mtu mmojammoja na jamii kwa ujumla.
“Serikali kwa kutambua kuwa Lishe ni suala la kimaendeleo hapa Nchini mapambano dhidi ya Lishe duni yamekuwa mojawapo ya maeneo ya kipaumbele katika mpango wa pili wa Maendeleo Kitaifa miaka mitano 2021 hadi 2026”.
Amesema mpango huo umejikita katika maeneo manne ikiwemo upungufu wa uzito,tatizo la vitamini na madini , uzito uliozidi na uliokithili nakuweka mazingira wezeshi katika utekelezaji wa shughuli za Lishe.
Ndumbaro amesema Serikali ya awamu ya sita inatambua Umuhimu wakuwekeza katika shughuli za Lishe kama msingi Imara na mkakati mojawapo wakufanikisha malengo na mkakati kupitia uchumi kwa maendeleo ya Viwanda ifikapo mwaka 2025.
Amesema Serikali kwa kutambua changamoto hizo ili kutoa msukumo wa kutekeleza afua za Lishe Nchini, kuunda na kuzindua utekelezaji wa mpango jumuishi waTaifa mwaka 2021 dadi2025,hivyo ametoa rai kwa waratibu hao kuhakikisha kupitia mafunzo hayo wakatatue changamoto za Lishe katika Halmashauri ya Madaba.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo Cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba.
Agosti 16,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa