Kanisa la Tanzania Assemblies Of God wamehimitimisha sikukuu ya wanawake inayofanyika kila Mwaka mwezi Machi kwa kufanya huduma mbalimbali ikiwemo kupeleka mahitaji katika vituo mbalimbali vya watoto yatima.
Kaniasa la Tanzania Assemblies of Madaba Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma wameadhimisha sherehe hizo kwa kufanya huduma mbalimbali ikiwemo kutoa mahitaji katika kituo cha watoto yatima Mahanje na kufanya huduma mbalimbali katika Kanisa.
Akisoma lisala katika Sherehe hizo Mhasibu wa Jimbo la Ruvuma Kati Rehema Haule amezisema changamoto zinazosababisha wanawake wa kanisa hilo kupelekea kutofanya huduma za Kimungu kwa usahihi ikiwemo majukumu mengi ya kujitafutia maisha.
Hata hivyo wameomba kupata semina za mara kwa mara ikiwemo semina za ndoa,malezi ya familia pamoja na kupata maombi ili waweze kutimiza agizo la Mungu kwa kila mwanamke.
Naye Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Obeid Mwasyika amewapongeza wanawake wa kanisa hilo kwa kufanya huduma nzuri ya kuona watoto yatima pamoja na kuhudumu za kanisa.
Hivyo Mchungaji ameahidi kufanya Semina kwa wanawake hao mara kwa mara pamoja na kuendelea kuwaombea ili waweze kufanya vizuri katika kanisa na katika familia zao.
“Nimekuwa nikiwaombea kila siku,mwanamke bila Mungu hawezi kushinda hivyo niwaombe mshikeni Mungu zaidi ili awasaidie katika kila mnalofanya”.
Na mwandishi wetu Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Machi 3,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa