Wananchi wa halmashauri ya Wilaya ya Madaba wametoa maoni yao na wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Watazania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Madaktari bingwa bobezi mpaka vijijini.
Wakitoa maoni hayo katika hospitali ya Wilaya ya Madaba ambako wamepwatiwa huduma za Afya za kibingwa Bernadi Mbilinyi amesema ujio wa madaktari bingwa umeleta mafanikio makubwa ikiwa wamefaidika na huduma ambazo zilishindikana katika matibabu ya kawaida.
“Wito wangu kwa Serikali huduma hizi tuwe tunaletewa mara kwa mara ili tuweze kunufaika na huduma hizo isiwe tu kwa watu wanaoishi karibu na hospitali ya Muhimbili,tunamshukuru Rais Samia kwa kutupunguzia safari ya kwenda mbali kutafuta huduma ya afya hasa kwa sisi watu wenye kipato cha chini”.
Naye Diwani viti maalum halmashauri ya Wilaya ya Madaba Vumilia Tawete ameishukuru Serikali kwa huduma ya mama na mtoto ikiwa kwa mara ya kwanza mzazi amefanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo.
Hata hivyo amesema Tawete amenufaika kwa huduma za kibingwa na amewakaribisha wananchi kuhakikisha wanakuja kupata huduma katika hospitali hiyo iliyo kamilika.
“Namimi nimenufaika wananchi wote mje mpate huduma katika hospitali ya Wilaya tumekagua kila mahali majengo yamekamilika na vifaa vyote vipo”.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 1,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa