WANANCHI zaidi ya 100 katika kitongoji cha kifaguro kata ya Lituta Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamepewa elimu ya afya ya mtoto kuanzia akiwa tumboni hadi anapozaliwa na kufikia miaka mitano.
Akizungumza na wananchi hao Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Madaba Asha Marua ametoa rai kwa wazazi kuwa wanapogundua wanaujauzito wahakikishe wanawahi katika kituo cha kutolea huduma za Afya ili waweze kupatiwa huduma na kupelekea kujifungua mtoto mwenye afya bora.
“Tulio wengi tunajisahau mama anajihisi mjamzito anakaa nyumbani mpaka miezi sita wakati mwingine hadi saba anakujakuanza kliniki hapo lazima azaliwe mtoto mwenye matatizo ya udumavu”.
Amesema mama anapokuwa mjamzito na kuanza kliniki mapema anapata huduma ya vitamini A na vidonge vya kuongeza damu.
“Nadhani mmeshasikia maranyingi mtu anajifungua mtoto ana mgongo wazi,mdomo sungura, kuzaa mtoto njiti na mtoto kufia tumboni hayo ni madhara ya kuchelewa kuhudhuria kliniki mara baada ya kupata ujauzito”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Juni 29,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa