Wanafunzi wa darasa la awali hadi darasa la nne katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wanatarajia kuanza kupimwa viwango vyao vya uoni na usikivu kuanzia Jumatatu Mei 13 hadi 19, 2024.
Akizungumza katika kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Afisa Elimu Msingi Saada Chwaya Zoezi hilo litafanyika katika Mikoa minne Mkoa wa Ruvuma, Mtwara,Mbeya na Iringa ili kubaini wanafunzi wenye changamoto ya kuona na kusikia.
“Zoezi hilo litafanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya AfyaOfisi ya Rais TAMISEMI na USAID kupitia mradi wa Jifunze uelewe”.
Kwa upande wake mratibu wa Jifunze uelewe Mkoa wa Ruvuma amesema wanafunzi watakao baishwa kuwa na changamoto za uoni na usikivu watachunguzwa zaidi kitaalam na kupatiwa afua stahiki vikiwemo visaidizi kama vile miwani na shimesikio vitakavyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la HOJA.
Naye Afisa Elimu Maalum Halmashauri ya Madaba Teddy Sanga amesema kuwa Halmashauri ina wanafunzi wengi wanaohitaji visaidizi katika uoni na usikivu hivyo zoezi hili litaboresha ujifunzaji wa wanafunzi litasaidia kuinua kiwango cha taalum kwa wanafunzi wote kuwa na mazingira sawa ya kujifunza.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei 10,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa