KUFUATIA maadhimisho ya Wiki ya Kupambana na Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele Halmashauri ya Madaba wametoa Elimu ya Magonjwa katika maeneo tofauti ikiwemo Chuo cha Afya ya Wanyama na uzalishaji Lita.
Mratibu wa Mgonjwa hayo Daktari Betty Mbawala akizungumza na Wanafunzi wa Chuo hicho amesema Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wanzee na Watoto wanaadhimisha wiki hii ikiwa katika ngazi za Halmshauri na Mikoa wanapaswa kutoa Elimu inayohusu magonjwa hayo katika maeneo tofauti
“Tunapotoa Elimu hiyo ya Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele inasaidia kujenga uelewa wa pamoja na namna ya kufanya,tusiendelee kuita hayapewi kipaumbele maana yanamadhara kwetu kama hatuta chukulia mkazo na kujua magonjwa hayo na kuyadhibiti”.
Mbawala ameyataja Magonjwa matano katika Nchi ya Tanzania ambayo hayapewi kipaumbele ukiwemo Ugonjwa wa Usumbi,Matende na Mabusha,Kichocho cha tumbo,Minyoo pamoja na Trakoma.
Hata hivyo ameelezea jinsi ya kutumia kinga tiba ambazo zinatolewa bure na Serikali ili kuhakikisha Jamii inaepuka kupata magonjwa hayo.
Meneja wa Chuo hicho Beata Balindile akizungumza mara baada ya wataalam wa Afya kutoa Elimu hiyo amesema na wanafunzi hao kuhakikisha wanapata dawa hizo kufuatia eneo hilo lina hatari ya kupata magonjwa hayo.
“Ndugu zangu mnapopata fursa hii ya kuweza kupata Dawa tena bure na mazingira yetu mmeyaona hakikisheni mnameza dawa”.
Balindile amesema kuwa athari za ugonjwa huo unaweza usijitokeze haraka na ikapelekea kuleta matatizo katika familia hapo baadae ikiwa Elimu imetolewa kila mmoja ameze dawa kwa wakati.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano halmashauri ya Madaba
Januari 29,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa