WANAFUNZI 72 katika Shule ya Msingi Lilondo Kata ya Wino Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamefanikiwa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2023.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Agnes Sanga akisoma taarifa katika Hafla fupi ya Kuwaaga wanafunzi hao amesema wanafunzi hao walianza darasa la kwanza Mwaka 2017 wakiwemo wanafunzi 78 wavulana 43 na wasichana 35.
Sanga amesema hadi kufikia Mwaka 2023 wamehitimu wanafunzi 72 ikiwa wavulana 41 na wasichana 31 .
Mkuu wa wa Shule amemshukuru Diwani wa Kata hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa kufanikisha Shughuli mbalimbali za maendeleo katika Shule ya Lilondo.
“Tunakushukuru Mh. Diwani wa Kata ya Wino,wazazi na walezi pamoja na wadau kwa ushirikiano wa kufankisha shughuli zote za maendeleo pamoja na kuchangia chakula cha mchana kwa wanafunzi”.
Hata hivyo Mwalimu amesema Shule hiyo inaupungufu wa walimu 8,ukosefu wa fedha za kukarabati nyumba 1 ya Mwalimu pamoja na shimo la choo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 21,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa