MGANGA Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Madaba Chacha Wambura amesema ujio wa Madaktari bingwa umepelekea wananchi kuhamasika kutibiwa kwa wingi katika hospitali hiyo.
Hayo amesema ikiwa ni ni siku ya tano ya utoaji wa huduma za kingwa katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba kuwa mpaka kufikia leo wangonjwa 296 wamepatiwa huduma.
“Tumenufaika kwa vitu vingi sana ukilinganisha na siku zingine tumekusanya mapato kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mbili hali hiyo ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Hata hivyo Wambura amesema katika hospitali hiyo ambapo huduma ambazo hazikuanza kutolewa pamoja na huduma ya wagonjwa wa ndani ikiwemo uzazi zimeanza kufanyika na upasuaji wa uzazi.
“Tunawakaribisha wananchi wote hospitali ya Wilaya inauwezo wa kuhudumia wagonjwa wengi na huduma zitaendelea kutolewa ikiwa nasi tumepata elimu ya kibingwa na ujuzi na tutaendelea kutoa huduma za kibingwa kulingana na kile walichotupatia”
Mganga mfawidhi amemshukuru Rais wajamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanzisha mpango wa Madaktari bingwa kushuka hadi ngazi ya halmashauri na kuwapunguzia wananchi kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 1,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa