Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imepandisha walimu madaraja kwa asilimia 90 kwa wote ambao walistahili na kumaliza zoezi hilo kwa wakati.
Hayo amesema Afisa elimu taaluma Devis Mwasi katika hafla ya kuwapongeza walimu hao na kutoa zawadi mbalimbali kama motisha kwa walimu na shule zilizofanya vizuri mwaka 2023.
Mwasi amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa kuwasimamia kwa ukaribu Walimu na kupelekea kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwa miaka sita mfululizo.
“Mara kadhaa umesema wewe ni mwalimu japo ni wakili na umezijua taratibu zote za elimu na hata tunapofanya shughuli za Kitaifa hujawa nyuma tunakushukuru kwa kutusimamia vema”.
Aidha Mwasi amewashukuru wakuu wa shule kuendelea kuweka mauhusiano mazuri na walimu na kuhakikisha wanakuwa na umoja ambao unapelekea matokeo mazuri kila Mwaka.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 10,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa