WALIMU wa shule za msingi na sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wameaswa kuzingatia kutimiza wajivu wao katika ufundishaji.
Hayo amesema Afisa elimu Mkoa wa Dodoma Vicent Kayombo akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Adolf Ndunguru katika kikao kilichojumuisha walimu wanapofundisha kuwa na mbinu na wanafunzi kuwa na utayari wakujifunza.
Aidha ametoa maelekezo kuwa shule zote zihakikishe wanalima mboga mboga badala yakupanda maua.
“Kila mwalimu ahakikishe anakuwa na kazi ya ziada ya kufanya muache kutegemea mshahara tu,msikate tamaa,tambueni Serikali inawajali na kuwaunga mkono”
Aidha Kayombo amesema Serikali imehakikisha walimu wanapanda madaraja ili kuhakikisha wanakuwa na moyo wa kujituma katika kufundisha.
“Serikali imesema ipo pamoja na nyie mkafanye mapinduzi tumewapandasha madaraja mkatimize wajibu wenu”
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Juni 1,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa