HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya mafunzo ya Manunuzi kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed akifungua mafunzo hayo amesema ni sehemu ya kukumbushana ikiwa mwaka wa fedha 2022/2023 umeisha na kuanza mwaka wa Fedha mpya 2023/2024 na kutathimini utekelezaji wa Miradi ambayo imetekelezwa kwa kipindi hicho.
Mkurugenzi amesema Miradi mingi inayotekelezwa inatoka katika ngazi ya Elimu ya Msingi na Sekondari zaidi ya Shilingi Bilioni 4 imepokelewa kwaajili ya ujenzi wa miradi hiyo.
“Hizo fedha zote tulizopokea nasema kama ni mtihani na matokeo yake kuona miundombinu imesimama kwa viwango na ubora unaotakiwa”
Hata hivyo Mohamed amesema baada ya kuangalia ubora wa miundombinu pamoja na kuzingatia utaratibu wa manunuzi kwa mujibu wa sheria,zilizowekwa katika fedha pamoja na ufuatiliaji .
Hata hivyo Mkurugenzi amesema mwaka wa fedha 2022/2023 unapoisha ni mwanzo wa ukaguzi wa mwaka mpya wa fedha 2023/2024 kwa kuangalia matumizi ya fedha zilizoletwa kwaajili ya Miundombinu yote.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halamshauri ya Madaba
Julai 27,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa