HALMASHAURI ya Madaba imegawa vishikwambi 131 kwa walimu awamu ya pili Sekondari na Msingi.
Akizungumza katika zoezi la mgawo wa vishikwambi umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Madaba Afisa Elimu Msingi Taddy Sanga amewaasa walimu kutumia vifaa hivyo kwa matumizi sahihi ya kufundishia na kujifunzia.
“Hivyo vishikwambi huruhusiwi kwenda navyo kwenye kumbi za starehe,kuingianavyo kwenye nyumba za wageni na matumizi mengine ambayo siyo sahihi kama Serikali ilivyoagiza”.
Kwa upande wake afisa Elimu msingi upande wa takwimu Raphael Kibiligi amesema Halmashauri ya Madaba inajumla ya walimu wa Msingi 202 maafisa Elimu Kata 8 walimu wa kuu 27 na walimu 167.
Naye afisa Elimu Sekondari Edward Wellah amesema walimu wa Sekondari katika Halmashauri hiyo mgawo wa kwanza walipata 78 na mgawo wa pili wamepata walimu 72.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa