MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile ametoa rai kwa wananchi wa Wilaya hiyo kulima zao la Ufuta ambalo halitumii mbolea na linapendwa kutumiwa na nchi za nje.
Hayo alisema alipofunga kikao cha utekelezaji wa afua za Lishe cha Robo ya nne Aprili- Juni 2023 kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Ndile amesema watumishi waache kutegemea mshahara badala yake wawekeze katika kilimo cha zao la ufuta ambalo litasaidia kuwawezesha kupata fedha za ziada.
Kwa upande wake mkuu wa Idara ya Kilimo Halmashauri ya Madaba Joseph Mrimi amesema katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamefanikiwa kuuza ufuta katika vyama vya Msingi tani 134,584 kwa kilo shilingi 3200/= na kupata shilingi Milioni 430,668,800/=,Soya imeuzwa tani 11,217 kwa shilingi 855 jumla ya shilingi Milioni 9,590,535/=.
Hata hivyo Mrimi amesema wakulima wamepata kiasi cha shilingi Milioni 426,832,508/= na Halmashauri imepata ushuru wa zaidi ya shilingi Milioni 10,497,681’5/=
“Kijiji cha Ifinga kimefanikiwa kuuza ufuta katika chama cha msingi IFINGA AMCOS Kilo 93,949,wakulima wamepata shilingi Milioni 292 ,463,237/=pamoja na Halmashauri imepata ushuru wa shilingi Milioni 7,046,175/= ”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai,18,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa