HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wameadhimisha siku ya wajane kwa kuwapa elimu ya kujua haki zao na elimu mbalimbali za kijamii.
Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri hiyo Mariam Sibuga amesema katika maadhimisho hayo yanafanyika kwalengo la kufanya uhamasishaji na kujua namna ya kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu.
“Tunafanya maadhimisho kwamaana wajane wajue haki zao na kupinga ukatili ambao ulikuwa unafanyika hapo awali”.
Aidha kauli mbiu ya mwaka 2024 inasema imarisha mfumo wa upatikanaji wa Nishati na kukuza uchumi wa wajane na familia.
Hata hivyo Sibuga ametoa rai kwa wanawake wajane kuanzisha vikundi ili waweze kujipatia mikopo kwaajili ya ufugaji,kilimo na kukuza uchumi wa familia zao.
“Naomba msikae kinyonge wala msiwewapweke sasahivi mambo yamebadilika tuachane na mila na desturi kandamizi zinazosababisha wajane wasiweze kujikwamua kiuchumi”.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Juni 27,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa