• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

WAHUDUMU wakujitolea Ruvuma wapewa msaada wa baiskeli 15

Posted on: June 30th, 2021

WAHUDUMU  15 wa  kujitolea ngazi ya Jamii  ambao wamekuwa wanafanyakazi ya kuwasaidia watoto wa kaya masikini 423 mkoani Ruvuma wamepewa msaada wa baiskeli ili kuwasaidia kutoa huduma kwa jamii.

Msaada huo umetolewa na Shirika la Social Action Trust Fund(SATF) kwa udhamini wa mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI(PEPFAR), kupitia mfuko wa Balozi wa Marekani nchini Tanzania.

Akitoa taarifa kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea ,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa SATF Dkt.Sylivia Ruambo amesema jumla ya shilingi milioni 3.7 zimetumika kununua na kusafirisha baskeli hizo hadi Songea.

Dkt.Ruambo amebainisha kuwa SATF inatekeleza mradi wa tuwalinde watoto katika Halmashauri tatu za Mkoa wa Ruvuma ambazo amezitaja kuwa ni Madaba,Songea na Nyasa na kwamba mradi huo ni wa mwaka mmoja.

“Mradi umelenga kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata huduma za elimu,afya,ulinzi na haki za mtoto pamoja na kuziwezesha kaya masikini  kujenga uwezo kiuchumi’’,alisisitiza Dkt.Ruambo.

Hata hivyo amesema,pamoja na shughuli nyingine,mradi huo uliwajengea uwezo wahudumu 15 wa kujitolea katika ngazi ya Kata ambao wamekuwa wanasaidia kuielimisha jamii kuhusu haki za mtoto na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Amesema,mradi umeamua kuwanunulia basikeli wahudumu hao ili kuwarahisishia usafiri na kuwafikia walengwa majumbani kwao.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi basikeli hizo,Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema ametoa rai kwa wahudumu hao kuzitunza basikeli hizo na kuendelea kuwatumikia walengwa kama mradi ulivyoelekeza.

“Natambua kazi yenu kwa sehemu kubwa ni ya kujitolea,hivyo nawaomba mtangulize  mbele maslahi ya jamii ili kuweza kutimiza adhima ya kuwahudumia’’,alisisitiza Mgema.

Mgema amelishukuru Shirika la SATF na PEPFAR kupitia ubalozi wa Marekani kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya mkoani Ruvuma ambako wanatekeleza mradi wa Tuwalinde ambao unahudumia watoto 423.

Naye Mwakilishi wa Balozi wa Marekani Jeremy Divis amesisitiza kuwa wapo tayari kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali yenye tija kwa jamii ukiwemo mradi wa tuwalinde ambao unatekelezwa pia mkoani Ruvuma.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Juni 29,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa